Al Ahly inaonekana walikuja na plan kwamba wapate goli halafu walilinde kwa maisha yao yote lakini bado nilikuwa naona mapungufu kwenye dhamira ya Al Ahly
1: Yes walifunga goli katika muda sahihi kabisa (ukifunga goli mapema linaharibu mipango ya mpinzani wako)
2: Lakini baada ya goli mabingwa wa Afrika , hata pasi nne kwao ilikuwa ngumu sana mali inapotea kirahisi lakini pia walikuwa hawana watu wa kutosha kuelekea mbele (rahisi kwa Simba kurejesha mpira katika himaya yao)
3: Hata pale ambapo waliamua kukaa nyuma 4-5-1 wakimuacha Modeste mbele peke yake, nikuambie mapungufu makubwa ya muundo huu?
4: Ukiacha mtu mmoja mbele lazima awe energetic, anajua kukaba kuanzia juu (Modeste hakufanya maana yake Inonga na Malone wanacheza huru) : mbili wingers wako lazima wawe wana track back lakini El Shahat na Tau wakuwa abiria.
Tatu distance kutoka mstari wa viungo na mabeki inatakiwa kuwa ndogo lakini haikuwa hivyo ndio maana Chama Kanoute Saido na Kibu walikuwa wanacheza sana" kwenye shimo "
Benchikha mpango wake ulikuwa kucheza zaidi katikati ya mstari wa ulinzi na kiungo wa Al Ahly: nikajiuliza kwanini hataki kushambulia nyuma ya Fullbacks wa Al Ahly? Kumbe nikakumbuka anawajua hawa (dhidi ya USM Alger) anajua udhaifu wao ni kufunga Space nyuma ya kiungo chao.
Kocha alifanikiwa lakini wachezaji hawakuwa wafanisi, kuna actions nzuri zilitengenezwa na kufunga lakini hazikufanyiwa kazi.
Kipindi cha pili ndio kabisa ni kama mazoezini tunasema " WASHAMBULIAJI Vs WALINZI. Al Ahly kama wamewaambia Simba "tufungeni kama mnaweza" ni Simba tu ambao walikuwa mipango sahihi na ufanisi: Pasi sahihi hakuna, Runs hakuna, maamuzi sahihi hakuna, umaliziaji hakuna na mechi ndio iliishia hapo.
NOTE
1: False 9 ya Simba mara kadhaa iliwachanganya sana mabeki wa kati wa Al Ahly (mpango mzuri wa Benchinkha)
2: Yule Golikipa wa Al Ahly .. El Shenawy amepata mrithi golini.
3: Ngoma alikosa runners , kuna pasi kipindi cha pili alikuwa anazitaka lakini hana runners
4: Kibu D anafanya vitu vingi kasoro umaliziaji, ni headache kukabiliana naye
5: Modeste? Mmh sijui slow sana
6: Abdelmonm kitasa
FT : Simba 0-1 Al Ahly
0 Comments